1 Chronicles 3

Wana Wa Daudi

1 aHawa ndio waliokuwa wana wa Daudi waliozaliwa huko Hebroni:
Mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni ambaye mama yake aliitwa Ahinoamu wa Yezreeli;
wa pili, Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili wa Karmeli;
2 bwa tatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa Maaka, binti Talmai mfalme wa Geshuri;
wa nne, Adoniya, ambaye mama yake alikuwa Hagithi;
3 cwa tano alikuwa Shefatia ambaye mama yake alikuwa Abitali;
wa sita alikuwa Ithreamu, aliyezaliwa na mke wake Egla.
4 dHawa sita walizaliwa huko Hebroni ambako Daudi alitawala kwa miaka saba na miezi sita.
Daudi alitawala Yerusalemu kwa miaka thelathini na mitatu,
5 enao hawa ndio watoto wa Daudi waliozaliwa huko Yerusalemu:

mkewe Bathsheba, binti Amieli, alimzalia Shamua,
Sawa na Shimea; maana yake ni Mashuhuri, Maarufu.
Shobabu, Nathani na Solomoni.
6Pia kulikuwa na wana wengine: Ibihari, Elishua, Elifeleti, 7Noga, Nefegi, Yafia, 8 gElishama, Eliada na Elifeleti; wote walikuwa tisa. 9 hHawa wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wale wana waliozaliwa na masuria. Naye Tamari alikuwa dada yao.

Wafalme Wa Yuda

10 iMwana wa Solomoni alikuwa Rehoboamu,
mwanawe huyo alikuwa Abiya,
mwanawe huyo alikuwa Yehoshafati,
mwanawe huyo alikuwa Asa,
11 jmwanawe huyo alikuwa Yehoramu,
mwanawe huyo alikuwa Ahazia,
mwanawe huyo alikuwa Yoashi,
12 kmwanawe huyo alikuwa Amazia,
mwanawe huyo alikuwa Azaria,
mwanawe huyo alikuwa Yothamu,
13mwanawe huyo alikuwa Ahazi,
mwanawe huyo alikuwa Hezekia,
mwanawe huyo alikuwa Manase,
14mwanawe huyo alikuwa Amoni
na mwanawe huyo alikuwa Yosia.
15 lWana wa Yosia walikuwa:
Yohanani mzaliwa wake wa kwanza,
Yehoyakimu mwanawe wa pili,
wa tatu Sedekia,
wa nne Shalumu.
16 mWalioingia mahali pa Yehoyakimu kama wafalme ni:
Yekonia mwanawe,
na Sedekia.

Ukoo Wa Kifalme Baada Ya Uhamisho

17 nHawa ndio waliokuwa wazao wa Yekonia aliyekuwa mateka:
Shealtieli mwanawe,
18 oMalkiramu, Pedaya, Shenasari, Yekamia, Hoshama na Nedabia.
19 pWana wa Pedaya walikuwa:
Zerubabeli na Shimei.
Wana wa Zerubabeli walikuwa:
Meshulamu na Hanania.
Shelomithi alikuwa dada yao.
20Pia walikuwepo wengine watano:
Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia na Yushab-Hesedi.
21Wazao wa Hanania walikuwa:
Pelatia na Yeshaya, na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.
22 qWazao wa Shekania:
Shemaya na wanawe:
Hatushi, Igali, Baria, Nearia na Shafati; jumla yao walikuwa sita.
23Wana wa Nearia walikuwa:
Elioenai, Hizkia na Azrikamu; jumla yao watatu.
24Wana wa Elioenai walikuwa:
Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohanani, Delaya na Anani; jumla yao wote saba.
Copyright information for SwhNEN